Mjini Kilwa Masoko kando ya bahari ya Hindi upo ufukwe mzuri na maarufu uitwao Jimbiza. Katika ufukwe huu anazaliwa kijana shujaa aitwae ISIHAKA. Isihaka ni kijana ambaye amezaliwa na kukua katika mazingira ambayo vijana wengi wa maeneo hayo wameyapitia.
Mbali na simulizi hii kuelezea mapito ya Isihaka katika Maisha, simulizi hii inagusa desturi, Imani, na mazingira ya kiuchumi na kielimu katika ukanda huu. Kupitia simulizi hii unapata mafumbo yaliyofumbuliwa, siri zilizofichuliwa na ustaarabu na ukarimu wa watu wa pwani hii.
Mwandishi wa kitabu hiki Ndugu Chamwingi Abdallah Mpondachuma ametaja maeneo na majina ya wahusika halisi na palipokuwa na ulazima ametumia majina mbadala bila ya kuathiri uhalisia wa simulizi hii.
Ukianza kuisoma simuizi hii hutapenda kupumzika hadi hapo simulizi hii inapofikia mwisho.